KIKAO cha dharura cha Uongozi wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, umeisimamisha kazi Sekretarieti nzima ya klabu. Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga
alisema kwamba maamuzi hayo yamefuatia kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika tangu saa leo
Waliofukuzwa ni Katibu Celestine Mwesigwa na Ofisa Habari, Louis Sendeu, kutokana na kile ilichoeleza utendaji usioridhisha.Wengine wanaokumbwa na sakata hilo ni Masoud Saad, aliyekuwa Ofisa Utawala, Philip Chifuka aliyekuwa Mhasibu na Hafidh Saleh aliyekuwa Meneja ambaye anahamishiwa kuwa afisa mipango.
“Tumesitisha mikataba ya sekretarieti nzima, pia tumefanya marekebisho, tumemtoa Meneja wa timu na muda si mrefu tutamtangaza Meneja mwingie pamoja na sekretarieti mpya,”alisema Sanga.
Pia wamesema watamuandikia barua kocha Tom Santifiet ya kumkumbusha wajibu wake na kuzingatia wajibu wake, kutozungumza na vyombo vya habari holela.
Maamuzi haya yanakuja baada ya Yanga kuanza vibaya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuambulia pointi moja tu katika mechi zake mbili za awali, kutokana na sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Jumamosi na Jumatano ikachapwa mabao 3-0 na Mtibwa Morogoro Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
No comments:
Post a Comment