Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, September 10, 2012

RHINO NA POLISI ZATOSHANA NGUVU

TIMU za Rhino na Polisi za Tabora  zinazoshiriki ligi daraja la kwanza juzi zilishindwa kutambiana kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa ni mahsusi kwa ajili ya kuzipatanisha timu hizo kutokana na uhasama uliokuwepo tangu siku nyingi almanusra usichezwe baada ya mwamuzi Maulid Mwikalo kugoma kuanzisha mchezo kutoka na uwanja kutokamilika kwani haukuwa na vibendera vya kona (corner flags).

Baada ya alama hizo muhimu kuweka  mchezo ulianza mnamo majira ya saa 11 jioni na mpira ulichezwa vizuri sana na timu zilimaliza uhasama kupitia kwa msuluhishi ambaye alikuwa ni mkuu wa mkoa wa Tabora.

Timu ya Polisi Tabora ikiongozwa na nahodha wao Shafii Dauda ambaye ndio waliomba timu zikutanishwe walijipatia bao dk ya 35 kupitia kwa Idd Kibwana na timu ya Rhino nayo ilijipatia bao dk 80 kupitia kwa Bonge Majdi chini ya nahodha wao makini MbWiga.

Timu hizi zilikuwa na uhasama wa muda mrefu sababu iliyopelekea msimu ulipita wakati wa mchezo wao wa ligi kutokea fujo.

Kocha wa timu ya Polisi Athuman Kilundumya alizungumza na Habari za michezo kwa njia ya simu alisema yeye haamini kuwa kwenye mpira kuna uhasama ila alikisifu kikosi chake kucheza vizuri japo ndio wametoka kwenye mazoezi magumu kwani wanajiandaa na ligi daraja la kwanza inayotegemewa kuanza hivi karibuni.

Naye kocha wa Rhino alisema anashukuru kupata mechi ya kirafiki kwani imemsaidia kujua kasoro kwenye timu yake ila aliwamwagia sifa waamuzi kwa kuchezesha kwa kufuata sheria 17. Waamuzi walimwagia sifa hizo ni Maulid Mwikalo wa kati, Athuman Juma na Omary Juma ambao ni waamuzi wasaidizi.

No comments:

Post a Comment