MECHI ya Simba na Yanga, ya mzunguko wa kwanza wa mashindano
ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu huu wa 2012/2013 utakaoanza Septemba 15
unatarajia kuoneshwa katika kituo cha runinga ya Super Sport.
Mechi hiyo itakayochezwa
Oktoba 3 itaonyeshwa kupitia kipindi cha Super Weekend sambamba na mechi
nyingine za mashindano hayo ya ligi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa
Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura, alisema kwa sasa
TFF ipo kwenye mazungumzo na Super Sport.
“Tupo kwenye mazungumzo na Lengo letu ni mashindano ya Ligi
tunapata udhamini wa kituo cha Super Sport na mechi zake kurushwa kupitia kituo
hicho,” alisema Wambura.
Mechi nyingine zitakazorushwa Super Sport ni mechi ya
Septemba 28 kati ya , Septemba 29 kati ya Simba na Prison, Septemba 30 na mechi
ya Oktoba 1.
No comments:
Post a Comment