Nahodha wa chuda F.C akipokea zawadi la kombe na mbunge wa viti maalum CUF |
Na Mwandishi wetu, Tanga
HATIMAYE
timu ya Chuda FC ya Chumbageni Jijini Tanga, imetwaa ubingwa wa
mashindano ya Haniu Cup, kwa kuichapa kwa mikwaju ya penati timu ya Jiwe
FC yenye maskani yake Tanga Sisi.
Fainali
hizo ambazo zilihudhuriwa na mamia ya wakazi wa Jiji la Tanga, zilikuwa
za aina yake ambapo hadi kipyenga cha mwisho kinapulizwa timu hizo
ziliweza kutoka sare ya bao 1-1.
Chuda,
ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo baada ya kuibuka na
ushindi wa mikwaju ya penati 4 kwa 1 hali iliyowafanya mashabiki wa timu
hiyo kutoka na shangwe uwanjani.
Akizungumza
katika mashindano hayo kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), alisema ni
muhimu kwa mkoa huo kuwa na kiwanja mbacho kitakuwa ni mahususi kwa
ajili ya kuibua vipaji wa soka mkoani humo.
No comments:
Post a Comment