Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za
kifo cha Katibu Mkuu mstaafu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC),
Erasto Zambi kilichotokea jana Septemba 26 mwaka huu jijini Dar es
Salaam kutokana na maradhi.
Zambi
ambaye anatarajiwa kuzikwa Jumapili Septemba 30 mwaka huu kabla ya
kuwa kiongozi TOC, kwa muda mrefu alikuwa mwalimu wa michezo katik Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo wanamichezo wengi hasa waliokuwa
wanafunzi katika chuo hicho wamepita kwake.
Msiba
huo ambao uko nyumbani kwake Ubungo Kibangu, Dar es Salaam ni pigo kwa
familia ya Zambi, TFF na wanamichezo kwa ujumla nchini kutokana na
mchango na mawazo aliyotoa kwa shirikisho wakati akiwa kiongozi wa TOC.
TFF
inatoa pole kwa familia ya Zambi, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na
uvumilivu katika kipindi hiki cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya
marehemu Zambi mahali pema peponi. Amina
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment