Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom inaingia raundi ya nne kesho kwa mechi za Super Weekend ambazo zitaoneshwa moja kwa moja (live)
na kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini.
Mechi
ya kwanza ambayo itachezwa kesho itakuwa kati ya Azam na JKT Ruvu
Stars. Mechi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itaanza
saa 1 kamili usiku kwa viingilio vya sh. 3,000 mzunguko, sh. 5,000 kwa
VIP C na VIP B wakati VIP A kiingilio kitakuwa sh. 10,000.
Septemba 29 mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Simba na Tanzania
Prisons itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11
kamili jioni. Yanga na African Lyon zitapambana Septemba 30
mwaka huu kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 11 kamili jioni.
Uwanja
wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam wenyewe utakuwa mwenyeji
wa mechi kati ya Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar itakayochezwa Oktoba 1
mwaka huu kuanza saa 10.30 jioni. Mechi ya mwisho ya Super Weekend
itachezwa Oktoba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
ikizikutanisha Yanga na Simba kuanzia saa 1 kamili usiku.
Kikosi cha Azam FC |
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao |
Kikosi cha JKT Ruvu |
No comments:
Post a Comment