Pambano hilo lilikuwa la raundi tatu Naseer Mafuru alionekana kuzidiwa raundi ya kwanza na kufanya mwamuzi kusimamisha mchezo ili kupatiwa huduma ya kwanza kwani alikuwa anavuja damu lakini raundi ya pili na ya tatu alizinduka na kuanza kurusha makonde mfululizo.
Michezo ya kg 56 iliyochezwa iliwakutanisha Mrisho Juma wa Dodoma alimshinda kwa pointi 4.1 Bashiri Salum wa Arusha, Husein Mnimbo wa Ngome alimpiga Bakari Msame wa Mbeya kwani ilibidi mwamuzi amwoko (RSCH), Eliyawinga John wa Kilimanjaro alimpiga kwa pointi 5.0 Mawazo Samwel wa Polisi
Nao Undule Langson wa Pwani na Thomas Soni walipata ushindi baada ya mwamuzi kusimamisha mchezo kuwanusuru wapinzani wao na Leeroy John wa Manyara na Frank Nicolaus wa Temeke walipata ushindi wa chee baada ya wapinzani wao kutotokea ulingoni na Alib Athuman wa Singida alimtwanga kwa pointi 5.0 Hamisi Mpili wa Ruvuma.
Michezo mingine kwa uzito wa kg 60 ni Jumanne Omari wa Temeke aliyempiga Mussa Kimweli wa Mbeya kwa pointi 4.1, Fabian Gaudence wa Dodoma alimpiga Peter Stanley kwa pointi 4.1, Issa Matumla Iddi Pialali walishinda baada ya mwamuzi kusimamisha mchezo dk 1 kwa sababu wapinzani wao walionekana hawamudu mchezo (RSCO) na James Mataiga wa Ruvuma alimpiga Hashim Mtupa kwa pointi 5.0 na Ismael Isack wa JKT alimpiga kwa KO dk 1.35 Mohamed Mlaani wa Morogoro.
Naye mjumbe wa Baraza la Michezo Tanzania Jamal Rwambow aliwaasa mabondia kurudisha heshima ya ngumi Tanzania kama ilivyokuwa awali.
Rwambow ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania Dioniz Malinzi kwenye ufunguzi wa michezo hiyo aliyasema hayo mbele ya mabondia 119 toka mikoa 18 ya Tanzania.
Pia alisema kila bondia acheze vizuri na kufuata sheria za mchezo huo ili ipatikane timu nzuri itakayowakilisha taifa kwenye michezo ya madola na michezo ya Afrika.
Katika hatua nyingine BMT wametoa shilingi milioni mbili (2,000,000) kusaidia kufanikisha mashindano hayo ambayo yanakabiliwa na ukata.
Add caption |
Add caption |
No comments:
Post a Comment