Bondia Said Hofu aliyevaa red akipambana na Emanuel Mogella, Said Hofu alishinda kwa RSCO |
Joseph Michael aliyevaa nyekundu akipambana na Fadhili Hassan aliyevaa blue kwenye ufunguzi wa mashindano ya ngumi ya Taifa uwanja wa ndani wa Taifa leo jioni |
HABARI ZA MICHEZO lilishuhudia mabondia Said Hofu wa JKT akipambana na bondia Emanuel Mogella ambao ulikuwa ni mchezo wa tatu baada ya michezo miwili kutochezwa kutokana na mabondia wake kutokuwepo uwanja.
Bondia Hemed Salum wa Mara alipewa ushindi baada ya mpinzani wake Halili Mnyani toka Morogoro kutofika ulingoni.
Hata hivyo mchezo uliompa ushindi Said Hofu ushindi mwamuzi alilazimika kusimamisha kutokana na bondia Emanuel Mogella kuweka kichwa. Kitaalamu wanasema Said alishinda kwa RSCO.(Referee stop contest outclass)
Mpambano mwingine ulimpambanisha Joseph Michael (Arusha) na Fadhili Hassan toka Pwani ambapo Joseph Michael alimshinda Fadhili Hassan toka Pwani. Tutaendelea kuwafahamisha matokeo ila hawa mabondia waliocheza ni kg 49.
No comments:
Post a Comment