Klabu
za Ligi Kuu ya Vodacom zimekubaliana kukutana na mdhamini (kampuni ya
simu za mkononi ya Vodacom) kuzungumzia kipengele cha mkataba wa ligi
hiyo kinachozuia kampuni nyingine za mawasiliano kudhamini timu
zinazocheza Ligi Kuu.
Maazimio
hayo yalifikiwa jana (Septemba 18 mwaka huu) katika kikao kati ya klabu
hizo na Kamati ya Ligi kilichofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wallace Karia.
Wengine waliohudhuria kikao hicho ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura.
Maazimio
mengine ya kikao hicho ni TFF kuiandikia barua African Lyon ambayo
itaipeleka kwa mdhamini wake (Zantel) ikielezea hatua hiyo ili
kusimamisha udhamini huo wakati ikisubiri matokeo ya mazungumzo kati ya
klabu hizo na mdhamini wa Ligi Kuu juu ya kipengele cha kuzuia
washindani wa Vodacom.
Katika
mkutano huo, watendaji wawili wa Kamati ya Ligi ambayo iko katika
kipindi cha mpito kuelekea kuundwa kwa Bodi ya Ligi walitambulishwa kwa
klabu hizo. Watendaji hao ni Silas Mwakibinga ambaye ni Ofisa Mtendaji
Mkuu (CEO) na Joel Balisidya ambaye ni Ofisa wa Ligi (LO).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment