Mchezaji wa Italian FC ya Chanika akikimbia na mpira huku mchezaji wa Hyper FC ya Gongolamboto wakati wa mchezo wa nusu fainali ambapo Italian walifungwa bao 1-0 |
Fainali hizi za vijana wa U-14 zitachezwa uwanja wa Chanika uliopo nje ya manispaa ya Ilala kuanzia saa 10.00 jioni na zinatarajiwa kuhudhuriwa na mashabiki wengi.
Timu ya Hyper Fc iliingia fainali baada ya kuifunga Italian Fc ya Chanika bao 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali uliochezwa uwanja huo wa Chanika na kuhudhuriwa na watazamaji wengi.
Nayo Anta Shobo wao waliifunga Kipawa Fc 4-1 na kufanikiwa kutinga fainali
Akizungumza na HABARI ZA MICHEZO, Mratibu wa Mashindano Abdallah Kinyogoli alisema mashindano yalianza kutimua vumbi Septemba mosi mwaka huu na jumla timu 8 za vijana wa umri wa chini ya miaka 14 zilishiriki.
"Mashindano yalikuwa mazuri na nashukuru lengo la kuibua na kuendeleza vipaji limefanikiwa na nategemea kuanzisha mashindano mengine ili kuwapa fursa wachezaji chipukizi kucheza michezo mingi ili wapate uzoefu" alisema Abdallah.
Bingwa atapata zawadi ya Mbuzi mwenye thamani ya 60,000 na mshindi wa pili atapata mpira mmoja
No comments:
Post a Comment