BONDIA Francis Cheka jana usiku alimpiga kwa KO bondia Karama Nyilawila kwenye pambano la raundi 12 la UBO
Cheka alimpiga Nyilawila kwa KO raundi ya sita alipomtwanga ngumi
iliyompeleka chini na kumfanya refa kumwehesabia lakini aliponyanyuka
aliamua kuvua gloves kuahashiria amekubali matokeo.
Cheka ambaye aliingia ulingoni bila mbwembwe alimwacha Nyilawila
ajifurahishe kwa kurusha makonde ambayo alikuwa anayakwepa hivyo
kumfanya pumzi kumwishia mapema.
Ilipotimu raundi ya tano Cheka alianza kurusha ngumi nzito nzito na
kufanya ukumbi kulipuka kwa kelele za kusema " Cheka ua huyo unampotezea
muda, maliza"
|
Karama Nyilawila akiwa amekaa baada ya kupokea konde takatifu kutoka kwa Francis Cheka |
|
Francis Cheka akipangua ngumi ya Karama Nyilawila |
|
Bondia Karama Nyilawila akiwa amemkumbatia Francis Cheka |
Karama ambaye aliingia ukumbi kwa mbwembwe huku akisindikizwa na mabausa alijikuta akiondoka mnyonge baada ya kuonjeshwa makonde ya haja.
No comments:
Post a Comment