AHMED ARAJIGA NA ALLY HAMDANI WATEULIWA KUCHEZESHA CHAN 2024


MAREFA wawili wa Tanzania, Ahmed Arajiga na Ally Hamdani Said wamejumuishwa katika orodha ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ya wasimamizi wa mechi walioteuliwa kwa ajili ya kuchezesha Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024 zinazotarajiwa kuanza Agosti 2 hadi 30, mwaka huu katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda.
Jumla ya wasimamizi wa mechi 70 wamechaguliwa, wakiwemo waamuzi 26, waamuzi wasaidizi 26, na Maafisa wa Mechi 18 wa Video (VMOs) wanaowakilisha zaidi ya Vyama 30 Wanachama wa CAF kote barani.
Orodha hiyo inaakisi kujitolea kwa CAF katika kuimarisha viwango vya wasimamizi kwa kuchanganya waamuzi waliobobea na wanaochipukia, wakiwemo wa kiike Bouchra Karboubi wa Morocco na Shamirah Nabadda wa Uganda upande wa marefa na Diana Chikotesha wa Zambia na Atezambong Fomo Carine wa Cameroon kwa waamuzi wasaidizi wazoefu.
Katika orodha hiyo kuna Maafisa wa Video za Mechi (VMOS) kama Mahmoud Ashour wa Misri, Samir Guezzaz wa Morocco na Ghorbal Mustapha wa Algeria, wakisisitiza umakini wa CAF kwenye usaidizi wa kiufundi wa hali ya juu wakati wa michuano hiyo.
Maafisa wote wa mechi wanatarajiwa kuwasili katika mataifa wenyeji kabla ya kuanza kwa maandalizi ya mwisho, ikiwa ni pamoja na warsha ya waamuzi wa kabla ya mechi itakayoshughulikia vikao vya kinadharia na vitendo ili kuendana na itifaki wasimamizi wa CAF na zana za kiteknolojia kama vile VAR.
Fainali za CHAN 2024 zitaanza kutimua vumbi Agosti 2 katika Majiji ya Nairobi, Dar es Salaam, Zanzibar na Kampala hadi Agosti 30.

ORODHA KAMILI YA MAAFISA WA MECHI ZA CHAN 2024

WAAMUZI
Adissa Abdoul Raphiou Ligali (Benin)
Messie Jessie Oved Nvoulou (Kongo)
Kpan Clement Franklin (Côte d’Ivoire)
Malala Kabanga Yannick (DR Congo)
Ahmed Nagy Mosa Mahmoud (Misri)
Tsegay Teklu Mogos (Eritrea)
Jammeh Lamin N. (Gambia)
Nyagrowa Dickens Mimisa (Kenya)
Ahmed Abdulrazg (Libya)
Diakhate Ousmane (Mali)
Milazare Patrice (Mauritius)
Loutfi Bekouassa (Algeria)
Diouf Adalbert (Senegal)
Jelly Chavani (Afrika Kusini)
Ahmed Arajiga (Tanzania)
Aklesso Gnama (Togo)
Melki Mehrez (Tunisia)
Lucky Razake Kasalirwe (Uganda)
Vincent Kabore (Burkina Faso)
Brahamou Sadou Ali (Niger)
Brighton Chimene (Zimbabwe)
Mefire Abdou Abdel (Kamerun)
Bouchra Karboubi (Morocco)
Shamirah Nabadda (Uganda)
Kech Chaf Mustapha (Morocco)
Houssam Benyahya (Algeria)

WAAMUZI WASAIDIZI
Ngila Guilain Bongele (DR Kongo)
Lucky Kegalogetswe (Botswana)
Sanou Habib Judicael Oumar (Burkina Faso)
Emery Niyongabo (Burundi)
Rodrigue Menye Mpele (Cameroon)
Amaldine Soulaimane (Comoro)
Alao Salim (Benin)
Fasika Biru Yehualashet (Ethiopia)
Jawo Abdul Aziz (Gambia)
Addy Roland Nii Dodoo (Ghana)
Mwangi Samuel Kuria (Kenya)
Joel Wonka Doe (Liberia)
Nassiri Hamza (Morocco)
Yacouba Abdoul Aziz (Niger)
Dieudonne Mutuyimana (Rwanda)
Omer Hamid Mohammed Ahmed (Sudan)
Wael Hanachi (Tunisia)
Ronald Katenya (Uganda)
Eleyeh Robleh (Djibouti)
Ettien Eba Medard (Côte d’Ivoire)
Abeigne Ndong Amos (Gabon)
Sirak Samuel (Eritrea)
Ally Hamdani Said (Tanzania)
Malondi Chany (Kongo)
Adel Abane (Algeria)
Diana Chikotesha (Zambia)

MAAFISA WA VIDEO ZA MECHI (VMOS)
Mahmoud Ashour (Misri)
Dahane Beida (Mauritania)
Lahlou Benbraham (Algeria)
Bamlak Tessema Weyesa (Ethiopia)
Samir Guezzaz (Morocco)
Hamza El Fariq (Morocco)
Issa Sy (Senegal)
Atcho Prierre Ghislain (Gabon)
Daniel Lareya (Ghana)
Abongile Tom (Afrika Kusini)
Yasir Abdalaziz (Sudan)
Viana Letticia (Eswatini)
Maria Rivet (Mauritius)
Akhona Makalima (Afrika Kusini)
Stephen Yiembe (Kenya)
Atezambong Fomo Carine (Kamerun)
Jermoumi Fatiha (Morocco)
Ghorbal Mustapha (Algeria)

No comments