UCHAGUZI WA SHIRIKISHO LA RIADHA TANZANIA -RT KUFANYIKA AGOSTI 2
UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT)utafanyika jijini Mwanza Agosti 2 mwaka huu,imeelezwa.
Rais wa RT, Silas Isangi alithibitisha jana kuwa uchaguzi utafanyika mwezi Agosti jijini Mwanza katika ukumbi utakaotangazwa baadae. “Ni kweli uchaguzi huo utafanyika mwezi huo kama ulivyosema na kamati ya uchaguzi
imeshatangazwa,”alisema Isangi.Isangi alisema Kamati ya Uchaguzi imeshateuliwa na inatarajia kukutana wiki ijayo (wiki hii) ndio itapanga siku ya kuanza kuchukua fomu kwa waotaka kugombea, Kamati ya Uchaguzi RT inaudwa na Leonard Thadeo, ambaye ni mwenyekiti, wakati makamu wa mwenyekiti ni wakili, Benjamin Karume, wajumbe ni Irine Mwasanga, Dk. Hamad Ndee, na Mussa Hassan Mazwazwa.
Wadau wengi wa mchezo wa riadha wameanza kuhasishana kuchukua fomu ili kupata viongozi wanaowataka watakaoleta maendeleo ya riadha
nchini. Uchaguzi wa RT umekuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa mchezoka, huku wamtaka .Awali, uchaguzi wa RT ulitakiwa ufanyike mapema mwaka huu, lakini haukufanyika sababu mchakato wa kukusanya maoni ya rasimu ya mabadili ya katiba ulikuwa ukiendelea.
Hivi karibuni Msajili wa Vyama na Mashirikisho ya Michezo nchini, Abeli Ngiragwa alipitisha mabadiliko ya Katiba ya RT baada ya kuigonga mihuri.

Post a Comment