Pages

Saturday, July 20, 2024

Yanga yaonja ladha ya Bundesliga





MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wamefungwa mabao 2-1 na timu ya Augsburg inanayocheza Ligi Kuu ya Ujerumani kwenye michuano ya Mpumalanga katika Uwanja wa Mbombela, Afrika Kusini leo.

Bao pekee la Yanga lilifungwa na mshambuliaji mpya wa timu hiyo Jean Baleke akimalizia kwa kichwa krosi iliyopigwa na Maxi Nzengeli katika dakika ya 87.

Augsburg walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 37 likifungwa na Mads Pederson kabla ya Philip Titz kufunga bao la pili dakika ya 81.

Huo ni mchezo wa kwanza katika michuano hiyo inayohusisha timu tatu ambazo ni Yanga, Augsburg kutoka Ujerumani na Tx Galaxy ya Afrika Kusini.

Mchezo wa pili wa michuano hiyo Yanga watacheza dhidi ya Tx Gallaxy, Julai 24, mwaka huu.

Timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani Dar es Salaam, watamaliza ziara yao Julai 28 ambapo watacheza dhidi ya Kaizer Chiefs kwenye michuano ya Toyota Cup. 

Aidha, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi aliutumia mchezo huo kuwajaribu wachezaji wake wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao.

Waliosajiliwa msimu huu ni Clatous Chama, Jean Baleke, Price Dube, Duke Abuya, Aziz Andabilwe, Chadack Boka na Khomeini Abubakar.

No comments:

Post a Comment