Pages

Saturday, July 20, 2024

Tanzania yapanda viwango Fifa

 


TANZANIA imepanda nafasi moja katika viwango vya ubora wa soka kutoka nafasi ya 114 hadi 113 katika viwango vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) vilivyotolewa jana.

Huo ni mwendelezo mzuri wa timu ya soka ya Taifa kufanya vizuri kwenye michezo yake kwani Mei mwaka huu ilipanda tena kwa nafasi nne kutoka 119 (Februari) hadi 115 ambavyo vilitolewa Mei mwaka huu.

Tanzania imepata pointi 1,175 sawa na mwezi uliopita baada ya Taifa Stars kucheza na Zambia mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 jijini Ndola na kushinda kwa bao 1-0.

Kwa upande wa nchi za Afrika Mashariki, Uganda imeshuka kwa nafasi moja, sasa ipo 96 kutoka 95 na Kenya imeendelea kubaki 108 licha ya kucheza michezo mitatu na kushinda miwili na kufungwa mmoja.

Kwa upande wa Afrika, Morocco imeendelea kushikilia usukani licha ya kushuka kwa nafasi mbili kwenye viwango vya dunia huku nafasi ya pili ikikamatwa na Senegal na nafasi ya tatu ni Misri.

Argentina imeendelea kushika nafasi ya kwanza duniani ikifuatiwa na Ufaransa na Hispania ya tatu ikiwa imepanda kwa nafasi tano, England inashika nafasi ya nne na Brazil inashika nafasi ya tano.

No comments:

Post a Comment