Pages

Wednesday, July 24, 2024

SIMBA YAZINDUA JEZI ZA MSIMU 2024/2025

 




UZINDUZI wa wiki ya Simba na jezi zinazotumika kwa msimu ujao umefanya mji wa Morogoro uliopambwa na milima kuwa rangi nyekundu na nyeupe baada ya mashabiki wat imu hiyo kuwasili.

Safari ilianzia Dar es Salaam saa 12:00 alfajiri kwa kutumia Reli ya Kisasa ya kimataifa (SGR), na kuwasili stesheni ya Morogoro saa 1:30 ikiwa na mashabiki na wananchama wa Simba wakiongozwa na Ofisa Mtendaji wa klabu hiyo Imani Kajula na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Ahmed Ally.

Jezi zitakazotumika msimu huu zilizinduliwa kwenye hifadhi ya Mikumi ambazo ni bluu, nyekundu na nyeupe baada ya msimu uliopita kuzinduliwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Msafara huo ulifika Mikumi saa 8:30 ambapo pia kulikuwa na mchezo wa kirafiki kati ya wafanyakazi wa hifadhi hiyo na viongozi wa Simba.

Ahmed alimtambulisha mwanamuziki wa kizazi kipya, Ali Kiba kuwa ndiye atatumbuiza kwenye Simba Day itakayofanyika Agosti 3, mwaka Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam ikiwa ni msimu wake wa pili kutumbuiza.

Simba ambayo iko kambini Misri siku hiyo itacheza mchezo wa kirafiki na APR ya Rwanda, kabla ya kucheza nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, Agosti 8, mwaka huu.

Imani Kajula, alisema wamefanya uzinduzi wa Wiki ya Simba katika mbuga ya Mikumi kwa ajili ya kutangaza utalii.

Viingilio vya kilele cha Simba Day, mzunguko ni Sh 5000, rangi ya chungwa Sh 10,000, VIP C, Sh 20,000, B Sh 30,000, A Sh 40,000 na Platinum Sh 200,000.

No comments:

Post a Comment