Pages

Wednesday, July 24, 2024

DUBE AIBEBA YANGA

 



YANGA imepata ushindi wa kwanza wa michuano ya Kombe la Mpumalanga baada ya kuafunga wenyeji wao Tx Galaxy kwa bao 1-0 katika Uwanja wa Mbombela, Afrika Kusini leo

Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na Prince Dube dakika ya 55 lakini pia Galaxy walipata penalti dakika ya 73, wakakosa.

Kwa matokeo hayo Yanga ina pointi tatu sawa na Augsburg ya Ujerumani ambao walishinda 2-1 dhidi ya Yanga.

Usajili mpya wa Yanga unaonekana kuwa na tija kwani mabao katika michezo yaote yamefungwa na Jean Baleke ambaye amesajiliwa kwa mkopo kutoka TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Dube kutoka Azam FC.

Yanga wanatumia michuano hiyo kama sehemu ya matayarisho ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa.

Yanga watakamilisha ziara yao nchini humo kwa kuikabili Kaizer Chiefs kwenye michuano ya Kombe la Toyota Julai 28 mwaka huu na wanatarajia kurejea nchini Julai 30 kwa maandalizi ya Kilele cha Wiki ya Mwanachi, Agosti 3, mwaka huu.

Mwisho

No comments:

Post a Comment