Fei Toto |
Aziz Ki |
TUZO ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania
Bara msimu wa 2023/2024 imeonekana kuwa na ushindani baada ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kutoa orodha ya wachezaji wanaowania tuzo
mbalimbali.
Katika tuzo hizo zitakazotolewa Agosti 1, mwaka huu Masaki, Dar es Salaam kipengele cha mchezaji bora kinawaniwa na wachezaji wanane ambao ni Stephane Aziz Ki, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Kipre Jr. Djigui Diarra, Ley Matampi, Yao Kouassi, Ibrahim Bacca na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.
Katika
kipengele cha kipa bora wa Ligi Kuu Tanzania Ayoub Lakred, Djigui Diarra na Ley
Matampi kwa upande wa mabeki ni Yao, Bacca na Tshabalala, tuzo ya kiungo bora
Aziz Ki, Fei Toto na Kipre Jr, kocha bora ni David Ouma, Bruno Ferry na Miguel
Gamondi.
Aziz Ki
huenda akatwaa tuzo zaidi ya moja kwa sababu tayari tuzo ya mfungaji bora wa
Ligi Kuu ni yake kwa kuwa anaongoza kwa kufunga mabao 21.
Pia Fei
Toto ana nafasi nzuri ya kuondoka tuzo, kwani alikuwa na msimu bora na
alimaliza ligi akishika nafasi ya pili katika ufungaji wa mabao akiweka kambani
mabao 19.
Aidha
tuzo zilijumuisha mashindano yote yaliyochini ya TFF kuanzia Ligi Kuu zote kwa
maana ya wanawake na wanaume, Championship, First League, soka la ufukweni,
Kombe la Shirikisho na Ligi ya Vijana ya U20.
Kadhalika
kutakuwepo na tuzo ya mchezaji bora anayecheza nje ya nchi wa kiume na
wanaowania ni Mbwana Samatta, Himid Mao na Novatus Dismas na kwa wanawake wapo
Opa Clement, Clara Luvanga na Aisha Masaka.
No comments:
Post a Comment