Pages

Wednesday, July 17, 2024

Simba kinara mapato mlangoni Ligi Kuu Tanzania Bara


 

KLABU ya Simba inaongoza kwa mapato ya milango kwa msimu wa 2023/2024.

Katika taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) leo inaonesha Simba iliingiza Sh 835,805,000 ikifuatiwa na Yanga Sh 825,065,000 na nafasi ya tatu ikashikiliwa na Tabora United kwa Sh 223,270,000.

Mashujaa iliingiza Sh 140,702,000, Singida Sh 135,045,000, Dodoma Jiji Sh 126,722,000, Geita Gold Sh 119,046,000, Tanzania Prisons Sh 118, 835,000, Azam FC Sh 116,048,000, Coastal Union Sh 102,509,000, KMC Sh 76,716,000.

Nyingine ni Ihefu Sh 62,106,000, Mtibwa Sugar Sh 51,698,000, Kagera Sugar Sh 46,703,000, Namungo FC Sh 32,525,000 na JKT Tanzania Sh 32,054,000.

No comments:

Post a Comment