Pages

Friday, September 8, 2023

Tamasha la michezo la Wanawake Oktoba 2023



Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha ambaye pia ni Mwenyekiti wq Kamati ya Tamasha la michezo kwa wanawake (Tanzanite) leo Septemba 08, 2023 ameongoza kikao cha kwanza cha Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika kwa awamu ya tatu  mwezi 0ktoba, 2023, Dar es salaam.


Tamasha la mwaka huu linalotarajiwa kufanyika kwa siku mbili  ambalo litahusisha mechi kali ya mpira wa miguu ya wanawake kwa siku ya kwanza ikifuatiwa na Kongamano kabambe litakalokuwa na mada mahususi kwa mustakabali wa kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo sambamba na tuzo kwa wanawake waliofanya vizuri katika sekta ya michezo.

No comments:

Post a Comment