Pages

Friday, September 8, 2023

TAIFA STARS YAFUZU AFCON 2023 LICHA YA KUTOKA SULUHU NA ALGERIA




 Timu ya soka ya wanaume ‘Taifa Stars’  imefuzu Michuano ya Mataifa Afrika kwa mara ya tatu, ‘AFCON 2023’ wakiwa ugenini dhidi ya Algeria, katika dimba la May 19, 1956 nchini Algeria.

Matokeo ya 0-0 ya dakika 90 yameifanya Stars kumaliza nafasi ya pili katika Kundi F, kwa pointi 8 nyuma ya Algeria vinara wa kundi wenye alama 16 hivyo timu mbili za juu zimekata tiketi ya kushirikia AFCON 2023 itakayovurumishwa huko Ivory Coast.

Majirani Uganda ‘The Cranes’ licha ya kupata ushindi wakiwa ugenini 0-2 dhidi ya Niger wamemaliza nafasi ya tatu wakiwa na pointi saba  na mkiani yupo Niger kwa pointi mbili.

No comments:

Post a Comment