Pages

Friday, September 8, 2023

RAIS SAMIA AIZAWADIA TAIFA STARS MILIONI 500/=



Rais Samia Suluhu Hassan, ametimiza ahadi ya kutoa Sh. milioni 500 ambazo aliahidi endapo timu hiyo itafuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 nchini Ivory Coast.


"Mtakumbuka wakati wa kujiandaa na mechi ya Uganda kule nyumbani, Rais alitoa ahadi ya kutoa Shilingi milioni 500, timu ikifuzu. Nafurahi kuwaambia kwamba hizo fedha sio tu kwamba zitatolewa, zimekwisha letwa Wizarani kwa ajili yenu”,  alisema Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Saidi Yakubu, wakati
akizungumza na Wachezaji na viongozi wa timu hiyo jana Septemba 7, 2023 nchini Algeria.

Pamoja na kuwaambia habari hiyo njema, Katibu Mkuu aliwapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa kazi kubwa waliyofanya akisema safari ya matokeo hayo haikuwa nyepesi hadi dakika ya mwisho.

No comments:

Post a Comment