TIMU za
Taifa za Soka za Vijana, zilizochini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys na
U-20, Ngorongoro Heroes leo zinatarajiwa kushuka viwanjani kucheza michezo ya
kimataifa.
Ngorongoro
heroes itakuwa nchini DR Congo kwenye mchezo wa marudiano wa kutafuta kufuzu
fainali za Afrika baada ya mchezo wa awali kutoka suluhu kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Kocha wa Ngorongoro Heroes’ Ammy Ninje wamejiandaa vema kwa mchezo huo na wachezai
wameahidi kucheza kufa ama kupona ili waweze kusonga mbele
"DRC ni timu ya kawaida kwani kama ni bora kuliko
Ngorongoro wangepata ushindi katika mchezo wa kwanza uliochezwa katika uwanja
wa Taifa Dar es Salaam, hivyo wasubiri kipigo katika mchezo wa kesho (leo) ," alisema Ninje.
Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ndio imegharamia
usafiri kwa timu ya Ngorongoro ambayo
iliondoka ikiwa na wachezaji 21 na benchi la ufundi ni watu saba
Nayo timu ya
Vijana waliochini ya miaka 17, Serengeti boys inatarajia kucheza mchezo wake wa
mwisho wa mashindano ya Cecafa katika hatua ya makundi dhidi ya Sudan katika mkoa wa Gitega kuanzia
saa 9:00 kwa saa za Burundi
Serengeti
boys ambayo ilikuwa katika kundi moja na Zanzibar ambayo iliondolewa kwenye
mashindano kwa madai ya kupeleka wachezaji ambao wamezidi umri inahitaji
ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu nusu fainali.
Akizungumza
jana Kocha wa timu hiyo Oscar Mirambo
alisema Serengeti boys ipo tayari kuhakikisha inaondoka na ushindi ili
ifuzu nusu fainali na wana ari kubwa hivyo wanatarajia kushinda mchezo huo.
“Mchezo na
Sudan ni muhimu kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri kwani ni mchezo wa
mwisho katika hatua ya makundi,” alisema Oscar
Nusu fainali
zitachezwa Aprili 24 na mchezo wa
kutafuta mshindi wa tatu utachezwa fainali zitachezwa Aprili 28katika Uwanja wa
Ngozi.
Mashindano
ya CECAFA U-17 yatashirikisha timu saba ambazo ni Uganda, Sudan, Burundi,
Kenya, Somalia na Ethiopia na Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment