Uhuru FM kwa kushirikiana na Dar-live itafanya show inayokwenda kwa jina
la MIC TATA itakayokutanisha miamba ya Muziki nchini.
Mratibu show hiyo Said Ambua, amesema
Wasanii watakaokutanishwa katika shown hiyo ya MIC TATA ni wa Bongo Flava,
Singeli, Taarabu na Hip Hop.
Aliwataja wasanii hao kuwa ni
Barnaba, Inspector Horun, Manfongo, Dulla Makabila, Joh Makini, ambapo kwa
upande wa taarabu ni Amigo ambaye alikuwa kwenye band ya Mzee Yusuph na kwa
sasa anajitengemea.
Alisema lengo la Show hiyo ni muendelezo wa
kampeni ya GUSA MAISHA YAO ambayo inalengo la kusaidia wasiojiweza kwa kile
kitakachopatikana.
Show hiyo itafanyika katika ukumbi wa
Dar-Live, Mbagala Zakyeem Februari 24 Mwaka huu kwa kiingilio cha shilling
5,000 kuanzia saa mbili za usiku.
Kampeni ya Gusa Maisha Yao ilianza mwaka
jana kwa kituo cha Uhuru Fm kutoa msaada katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,
kuchangia damu, na kutoa msaada kituo cha waathirika wa dawa za kulenya.
No comments:
Post a Comment