Pages

Friday, September 29, 2017

KIM POULSEN AITA 50 NGORONGORO HEROES


KOCHA Mkuu wa timu za Vijana, Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 50 wa timu ya taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ ambao wanatarajia kuingia kambini Oktoba Mosi.
Akizungumza Poulsen alisema timu hiyo inaundwa na wachezaji na wachezaji waliokuwa Serengeti boys iliyoshiriki AFCON yaliyofanyika Gabon, mashindano ya timu za U-20 na wengine wnatokana na mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA.
 “Kuna wachezaji 23 wa timu ya Serengeti Boys iliyoshiriki fainali za Gabon mwaka huu na walifanya vizuri na sasa natarajia watafanya vizuri na kati ya hao 50 nitawachuja ili kupata wachezaji 30 ambao wataunda kikosi cha Ngorongoro Heroes,” alisema Poulsen.
Pia Poulsen alisema wapo hata wachezaji hawakubahatika kwenda Gabon kutokana na umri kuzidi na watafanya mazoezi pamoja kabla ya kuwachuja kupata wachezaji 30 ambao watakuwa wanaingia kambini kila mwezi.
Kambi hii itakuwa ya wiki mbili ambapo wachezaji hao watakuwa chini ya kocha Kim Poulsen, msaidizi wake Oscar Mirambo na kocha wa makipa Peter Manyika.
Awali akizungumza Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas alisema TFF imemteua Poulsen kuwa kocha mkuu wa timu za vijana za Serengeti boys, Ngorongoro heroes na Kilimanjaro.

Awali Poulsen katika uongozi wa TFF uliopita alikuwa mshauri wa ufundi wa timu hizo na kocha alikuwa Bakari Shime kibarua ambacho kinaonekana kuota mbawa kwake kwa sasa.

No comments:

Post a Comment