Pages

Thursday, September 28, 2017

SERIKALI IPO TAYARI KWA MASHINDANO YA VIJANA YA AFRIKA 2019




SERIKALI imesema ipo tayari kwa ajili ya kuwa wenyeji wa mashindano ya Vijana ya Afrika waliochini ya Umri wa miaka 17 (AFCON U-17) yanayotarajiwa kufanyika 2019 hivyo Watanzania wasiwe na wasiwasi.
Hayo yalisemwa leo na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe wakati akipokea taarifa ya maandalizi kutoka Shikirisho la Soka Tanzania (TFF) hafla iliyofanyika Dar es Salaam.
‘Sisi wenyewe serikali ndio tuliandika barua Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF)  na kusema tunaomba kuandaa fainali za Vijana za Afrika kama nchi zingine zinavyofanya na mwaka 2015 tulikubaliwa,”  alisema Dk. Mwakyembe.
Alisema anashukuru kuona maandalizi yalianza mapema na sasa Tanzania ina timu nzuri ambayo inatarajiwa kuleta ushindani na kusema usalama wa kutosha upo, hoteli na barabara zitakazopita magari wakati wa kwenda uwanjani na mazoezini zinafanyiwa kazi.
 “Jana (juzi) nilitembelea Uwanja wa Taifa ambao upo kwenye marekebisho na sasa unaendelea vizuri na nataka ukikamilika utiwe kufuli wakati tunaendelea na kuandaa viwanja vingine,” alisema Dk. Mwakyembe
Pia alisema sehemu ya vyumba vya kubadilishia nguo imekamilika na kusema kutakuwepo na hoteli ndani ya uwanja wa Taifa ambayo itakuwa inatoa huduma kipindi chote na kusema ataendelea kushirikiana na sekta binafsi kuona fainali hizo zinafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Dk. Mwakyembe alitumia fursa hiyo kumpongeza mjumbe wa heshima wa CAF, Leodgar Tenga kwa namna ambavyo amekuwa akiiwakilisha vema Tanzania katika soka kwani amekuwa akitetea nchi za
Awali akizungumza, Mjumbe wa heshima wa Caf, Leodgar Tenga alisema kwa asilimia kubwa Tanzania imefanya maandalizi makubwa na ana uhakika sasa mashindano yatafanyika
 ‘’Sisi wengine tunaona fahari kuandaa mashindano haya kwani nchi haijawahi kufanya hivyo, na CAF wana matumaini makubwa maana tuna uwanja mzuri, tuna mashabiki na sifa ya amani nayo inatupaisha,” alisema Tenga.
Tenga alisema Caf ina uhakika mashabiki watakuja na kurejea  chini mwao wakiwa salama kwa sababu Tanzania ni nchi ya amani nanajisikia fahari kuwa sehemu yake.
Aidha Tenga alisema CAF imepandisha viwango kwa ajili ya kupandisha soka la Afrika hivyo kufanikiwa kuandaa fainali za vijana itasaidia kuitangaza nchi na bara la Afrika.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mkurungenzi wa Maendeleo ya Michezo Dk. Yusuph Singo, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wallace Karia, , Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred, Mkurengezi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi, Henry Tandau, Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kasongo na wajumbe wa kamati ya ufundi

No comments:

Post a Comment