Pages

Saturday, September 16, 2017

KAMPENI YA UZALENDO KWANZA YAMKUMBUKA ATHUMAN HAMIS, WACHEZAJI WA ZAMANI WAJIUNGA NAO




Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo kwanza Steve Mengele ‘Steve Nyerere’ akimkabidhi moja ya sehemu ya msaada wa vyakula mbalimbali kwa aliyewahi kuwa mpiga picha wa Magazeti ya Serikali (Habari Leo &Daily News),Athuman Hamis (katikati) ambaye alipata ulemavu wa kudumu kufuatia ajali aliyoipata akiwa kwenye majukumu yake ikiwa yapata miaka kumi sasa. Anayepokea ni Msafiri Athuman ambaye ni mtoto wake.



Baadhi ya Wasanii mbalimbali wa Bongo movie wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri





Baadhi ya Wasanii mbalimbali wa Bongo movie wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri

Wachezaji wa Soka wa zamani waliosimama wakati wakitambulishwa.



Wasanii wakimsaidia Athuman Hamis kupanda ngazi




KAMPENI ya Uzalendo Kwanza iliyoanzishwa na wasanii wa filamu nchini ‘Bongo Muvi’  imezidi kutanua wigo baada ya jana kuongezeka matawi mikoa yote ya Tanzania na wachezaji wakongwe waliowahi kutamba kwenye Soka wakijiunga.
Akizungumza wakati akiwapokea wanachama wapya, Mwenyekiti, Steve Mengele 'Steve Nyerere' alisema lengo ni kuwafikia Watanzania wote ili wafahamu umuhimu wa uzalendo, kuipenda nchi yao pamoja na kushirikiana na serikali ya awamu ya tano ya Rais John Pombe Magufuli kumuunga mkono kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kimaendeleo.
"Taifa la wazalendo linaanzia darasani, tunawaomba walimu wawe wazalendo kufundisha darasani, manesi na madakatari wawe wazalendo kutoa huduma, uzalendo pia ni muhimu kusapoti klabu zetu za soka na timu ya Taifa na wasanii wa muziki ni lazima wawe wazalendo kwa kuitangaza nchi kwa mambo ya Kizalendo," alisema Nyerere.
Wachezaji wa soka ambao walijiunga na Uzalendo Kwanza ni Mwanamtwa Kihwelo, Ramadhan Kampira, Monja Liseki, Abdallah Kaburu, Dotto Mokili na wengine.
Aidha Nyerere amewaasa wasanii hao na Watanzania kuunganisha nguvu ya pamoja ili kulinda kazi zao za sanaa sambamba na Watanzania kupenda kununua kazi za wasanii wa ndani ili kukuza kipato chao na kuinua uchumi wa nchi.
Mbali na hao, msanii wa Bongo Fleva, Ruby alijiunga na kampeni ya Uzalendo Kwanza nakupewa jukumu la kutunga nyimbo za Uzalendo na video zake ili kufikisha ujumbe kwa wananchi wote.
Katika hatua nyingine,uongozi wa Uzalendo kwanza umetoa msaada wa vyakula mbalimbali na kiasi cha fedha tasilimu shilingi laki tano kwa aliyewahi kuwa mpiga picha wa Magazeti ya Serikali (Habari Leo &Daily News),Athuman Hamis ambaye alipata ulemavu wa kudumu kufuatia ajali aliyoipata akiwa kwenye majukumu ya kazi yapata miaka kumi na mlemavu mwingine akipewa baiskeli.
Steve Nyerere aliwakumbusha wasanii kujiunga katika mifuko ya hifadhi ya kijamii na alisema mfuko wa hifadhi ya Jamii PPF wameanza kwa kuidhamini kampeni ya Uzalendo Kwanza na wameonesha utayari kuwasaidia iwapo watajiunga katika mfuko huo.




No comments:

Post a Comment