Pages

Wednesday, September 13, 2017

DRFA YAGAWA MIPIRA 200 LEO


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam, (DRFA) Salum Mwaking’inda (katikati) akimkabidhi mipira Katibu wa Chama cha Soka Ilala (IDFA) Daud Kanuti (kushoto) hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. Kulia ni Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Shirikisho la mpira wa miguu (TFF) kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, Lameck Nyambaya (Picha na Rahel Pallangyo)






CHAMA cha Soka cha Mkoa wa Dar es Salaam kimegawa mipira 200 kwa vituo vya soka vilivyopo katika wilaya za Ilala, Kinondoni, Temeke, Kigamboni na Ubungo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mipira hiyo, Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Shirikisho la mpira wa miguu (TFF) kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, Lameck Nyambaya aliishukuru TFF kwa kuwapatia mipira 200 ambapo kila wilaya itapata mipira 40
“Nashukuru TFF kwa kuona umuhimu wa kuongezea Dar es Salaam mipira kwani mikoa mingine ilipatiwa mipira 100 lakini sisi tumepewa 200 ambayo tunaigawa na baadae nitafuatilia kuona kama imepelekwa katika vituo,” alisema Kambaya
Pia Kambaya alisema kupatikana kwa mipira hiyo itasaidia Dar es Salaam kuendelea kutoa wachezaji bora kwenye ligi mbalimbali.
Naye MakamuMwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam, Salum Mwaking’inda alishukuru kupata mipira hiyo na kusema wataigawa kwa usawa katika vituo vyote vya soka vilivyopo mkoa wa Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment