Pages

Wednesday, September 13, 2017

OMOG KUTUMIA MABEKI KUSHAMBULIA




KOCHA wa Simba, Joseph Omog katika kutatua tatizo la umalizia wa safu ya ushambuliaji ameibadilishia mfumo Mwadui FC na sasa inaonekana atatumia zaidi mabeki wa pembeni kuanzisha mashambulizi  na mawinga wakiingia kati kujumuika na washambuliaji kumalizia.
Hayo yalionekana katika mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jana na leo kocha Omog alitumia zaidi ya dakika 30 kuwaelekeza mabeki Ally Shomari na Mohammed Hussein kuanzisha kwa kasi mashambulizi kutoka pembeni na kupiga krosi kwa washambuliaji John Bocco na Emmanuel Okwi huku mawinga Shiza Kichuya na Mohammed Ibrahim nao wakiingia ndani.
Katika mazoezi hayo Omog alionyesha msisitizo kwa mabeki hao wa pembeni ambapo kuna kipindi alililazimika kuwa mkali pale wachezaji hao waliposhindwa kufanyika kiufasaha hali iliyoonyesha amedhamiria kupata pointi tatu katika mchezo unatakaochezwa Jumapili ijayo.
Katika kuonesha msisisizo kocha Omog alikuwa anaonesha kwa vitendo kile alichohitaji kufanyika na kumfanya kugongana kwa bahati mbaya na mshambuliaji wake Okwi na kuumia kwenye jicho na kupewa huduma ya kwanza na daktari Yassin Gembe.
Mchezo uliopita Simba ilitoka suluhu na na Azam FC uliochezwa Jumamosi  iliyopita hali iliyomfanya Omog kubadili mfumo kwani washambuliaji walionekana kuwa butu
Kocha Omog alikigawa kikosi chake katika makundi mawili, kikosi cha kwanza kiliundwa na Aishi Manula, Ally Shomari, Mohammed Hussein, Juuko Murshid, Salim Mbonde, James Kotei, Shiza Kichuya, Said Ndemla, John Bocco, Emanuel Okwi na Mohammed Ibrahim.
Kikosi cha pili kilikuwa na kipa Emmanuel Mseja, Muharam Mohammed ambaye ni kocha wa makipa, Jamal Mwambeleko, Jonas Mkude, Yusuph Mpilipili, Mzamiru Yassin, Jamal Mnyate, Mwinyi Kazimoto, Laudit Mavugo na Nicholas Gyan.
Katika mazoezi hayo kikosi A kilishinda mabao 2-1 yaliyofungwa na Okwi na Bocco na kikosi B lilifungwa na Gyan.

No comments:

Post a Comment