Pages

Thursday, August 31, 2017

KOZI ZA UKOCHA ZA LESENI A, B NA C ZASITISHWA NA CAF



SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF) limesitisha kozi zote za makocha kwa nchi wanachama hadi mtaala mpya utakapotoka.
Akizungumza na wandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  Salum Madadi alisema CAF imesimamisha kozi za leseni C, B na A kwa ajili ya kuweka/kuandaa mtaala mpya.
“Tunaomba wale wote ambao walikuwa wamejiandikisha na kulipa ada kwa ajili ya kozi mojawapo wawe wavumilivu mpaka hapo tutakapopata maelekezo toka CAF,” alisema Madadi
Pia Madadi alitumia fursa hiyo kuomba radhi kwa hatua hiyo ya Caf.
Aidha kamati ya Ufundi ya TFF inatarajiwa kukutana Septemba 24 kuona namna ya kuendesha kozi hizo kwa wale ambao walikuwa tayari wameshalipa.

No comments:

Post a Comment