Pages

Sunday, August 27, 2017

FAINALI ZA WATOTO WA COMPASSION ZAFANA

Fainali za mashindano ya watoto kutoka Vituo vya Huduma ya Mtoto (Compassion) Kanda ya Mwanza zimefana baada ya kufikia tamati hii leo jumamosi Agosti 26,2017 kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Mashindano hayo yalianza tangu Mei 20 mwaka huu kwa kuhusisha michezo mbalimbali ikiwemo riadha, mpira wa miguu na mpia wa pete kwa lengo la kuibua na kuendeleza vipaji. Katika mchezo wa mpira wa miguu kwa wachezaji wenye umri kati ya miaka 14 hadi 18, timu ya Anglikana Igoma imeibuka bingwa baada ya kuilaza timu ya Moraviani Kigoto kwa bao 3-1 huku mshindi wa tatu ikiwa ni timu ya PAGT Mabatini iliyoilaza timu ya AICT Bujora kwa mikwaju ya penati 3-1 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika kipindi cha dakika 90. Bingwa kwa upande wa watoto wenye umri kati ya miaka minane hadi 12 ikiwa ni timu ya EAGT Buzuruga iliyoicharaza pia timu ya AICT Buhongwa kwa bao 3-1. Katika mpira wa pete timu ya wasichana wenye umri kati ya miaka 14 hadi 18 ya Anglikana Igoma imeilaza timu ya TAG Nyakato kwa magoli 47-41 na hivyo kuibuka bingwa huku timu ya Moraviani Kigoto ikiibuka mshindi wa tatu baada ya kuilaza timu ya FPCT Pasiansi kwa mabao 62-25. Nayo timu ya pete ya wasichana wenye umri kati ya miaka minane hadi 12 timu ya AICT Buhongwa imeibuka bingwa kwa mabao 14-11 dhidi ya timu yaEAGT Buzuruga. Katika fainali hizo, mgeni rasmi alikuwa Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Ilemela, Sarah Nthangu ambaye amekabidhi zawadi za vikombe na jezi kwa timu zilizoshinda pamoja na washindi wengine kwa upande wa mchezo wa riadha.
Tazama video hapo chini
] Nahodha wa timu ya Anglikana Igoma akipokea kombe baada ya timu hiyo kuibuka mshindi kwenye mashindano hayo Mgeni rasmi akimkabidhi jezi mshindi wa kukata upepo (riadha)
Mmoja wa washindi wa riadha akipokea zawadi Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Ilemela, Sarah Nthangu ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza baada ya michuano hiyo Berekia Erasto kutoka FPCT Pasiansi akisoma risala kwa mgeni rasmi Wachezaji wa Anglikana Igoma (kushoto), Moraviani Kigoto (kulia) pamoja na waamuzi

No comments:

Post a Comment