Pages

Sunday, August 27, 2017

Bao moja kila baada ya dakika 37 mechi za jana ligi kuu


 
MABAO 17 yamefungwa katika siku ya kwanza ya ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2017/18 katika mechi saba zilizopigwa ambazo ni sawa na dakika 630 na kufanya wastani bao moja kila baada ya dakika 37.
Mchezo wa Simba dhidi ya Ruvu Shooting uliopigwa katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ndio uliozalisha mabao mengi zaidi kufuatia Wekundu hao kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 huku mshambuliaji Emmanuel Okwi akifunga mabao manne peke yake.
Singida United ambayo ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutokana na usajili mkubwa iliyofanya kwa wachezaji wa ndani na nje wameanza kwa kupokea kipigo cha mabao 2-1 mbele Mwadui FC katika uwanja wa Mwadui Complex.

Wageni wengine wa ligi timu ya Njombe Mji nayo imeanza kwa kipigo kufuatia kufungwa mabao 2-1 nyumbani na Tanzania Prisons katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
Kesho kutakuwa na mchezo mmoja utakaopigwa katika uwanja wa Uhuru kati ya mabingwa watetezi Yanga dhidi ya Lipuli kutoka mkoani Iringa.
Matokeo kamili ya mechi za ligi zilizopigwa leo ni kama ifuatavyo:
Simba 7 vs 0 Ruvu Shooting
Ndanda FC 0 vs 1 Azam FC
Mwadui FC 2 vs 1 Singida United
Kagera Sugar 0 vs 1 Mbao FC
Mtibwa Sugar 1 vs 0 Stand United
Njombe Mji 1 vs 2 Tanzania Prison
Mbeya City 1 vs 0 Majimaji

No comments:

Post a Comment