Pages

Saturday, June 17, 2017

UCHAGUZI WA TWFA JULAI 8, FOMU KUANZA KUTOLEWA KESHO KUTWA



FOMU za kuomba uongozi katika Chama cha Soka la Wanawake (TWFA) zinatarajiwa kuanza kutolewa Juni 19 katika ofisi za Hosteli ya TFF, Karume na uchaguzi utafanyika Julai 8.

Akizungumza na wandishi wa habari juzi Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, George Mushumba alisema nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu Msaidizi fomu zitanunuliwa kwa Sh 200,000 wakati nafasi za Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji fomu zitapoatikana kwa Sh 100,000.

“Fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi zitaanza kutolewa Juni 19, mwaka huu na kwamba mwisho wa kuchukua na kurudisha ni Juni 22, mwaka huu saa 10.00 jioni,” alisema Mushumba.

Juni 23, Kamati itapitia majina ya wagombea walioomba kugombea nafasi mbalimbali na Juni 24 Kamati itatangaza majina ya wagombea waliostahili au waliotimiza taratibu za uchaguzi kwa mujibu wa katiba au kanuni za TWFA.

Juni 26 na 27, itapokea pingamizi kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni na Juni 28 kamati itapitia pingamizi.
Juni 29 kamati itatoa majumuisho ya pingamizi kama ziliwasilishwa na wadau na Juni 30 NI usaili kwa wagombea waliotangazwa

Julai Mosi kutangaza majina ya wagombea waliopitishwa, Julai 02, kamati kupokea rufaa, Julai 03 kamati kupitia rufaa kama zimewasilishwa

Julai 04 kamati kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea, Julai 04 hadi 07 wagombea kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili na  Julai 08 uchaguzi Mkuu wa TWFA

Mushumba alisema nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji na sifa ya elimu kwa wagombea wote ni kidato cha nne.

No comments:

Post a Comment