Pages

Saturday, June 17, 2017

MKUDE ATANGAZIWA DAU KUBWA YANGA


HII sasa ni vurugu! Baada ya kukamilisha usajili wa Ibrahim Ajibu, mabingwa wa ligi kuu Yanga wameendeleza ‘fujo’ zao safari hii wakimtangazia dau la kufuru nahodha wa Simba Jonas Mkude.
Taarifa za uhakika toka kwa mtu wa karibu wa Mkude zinasema kiungo huyo aliye kwenye mazungumzo na klabu yake ya Simba amepokea ofa ya sh 85 milioni pamoja na gari ya kutembelea kama atakuwa tayari kusaini mkataba wa miaka miwili Jangwani.
Taarifa zaidi zinadai kuwa kiungo huyo anaipa nafasi ya kwanza Simba ingawa kasi yao ndogo katika kufikia muafaka inaweza kumbadili mawazo na kuchangamkia donge nono la Yanga ambao wamemwachia mlango wazi ili muda wowote atakaokuwa tayari wamalize kazi.

Kama Simba itampoteza kiungo huyo kipenzi cha Wanamsimbazi litakuwa pigo jingine kubwa kwa wanazi wa timu hiyo ambao hadi leo hawaamini kama kweli Ajibu hatovaa jezi nyekundu msimu ujao.
Taarifa za kurejea kwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kwenye timu hiyo kumeongeza ugumu wa vita ya usajili ambayo hapo awali ilitawaliwa na Singida United kabla Simba kuliamsha ‘dude’ kwa kusajili nyota kadhaa katika kipindi kifupi.

No comments:

Post a Comment