Pages

Monday, June 26, 2017

OKWI ASAINI MIAKA MIWILI

Mshambuliaji wa kimataifa Emmanuel Okwi amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu ya Simba katika michuano mbalimbali kuanzia msimu ujao.
Okwi amesaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa kombe la FA mbele ya Makamu wa Rais wa klabu hiyo Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na mwanachama maarufu bilionea Mohamed Dewji ‘Mo’ usiku huu.
Raia huyo wa Uganda aliwasili nchini jana usiku ambapo ilitarajiwa kusaini mkataba mchana wa leo lakini mazungumzo baina yake na viongozi yalikuwa hayajakamilika na hatimaye usiku huu akakamilisha dili hilo.
Okwi akiwa na Mohamed Dewji ‘Mo’
Okwi anaungana na nyota wengine kama John Bocco ‘Adebayor’, Shomari Kapombe, Ally Shomari, Jamal Mwambeleko, Yusuph Mlipili na Emmanuel Mseja kwa ajili ya kuwatumikia Wekundu hao msimu ujao.
Simba inaandaa kikosi imara kwakua mwakani itashiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

No comments:

Post a Comment