Pages
▼
Monday, June 26, 2017
MOHAMED SALAH ASAINI LIVERPOOL
Liverpool wamekamilisha Uhamisho wa Gharama ya Pauni Milioni 34 kwa kumsaini Mchezaji wa zamani wa Chelsea anaechezea AS Roma ya Italy Mohamed Salah.
Salah, Raia wa Egypt mwenye Miaka 25, amesaini Mkataba wa Miaka Mitano na kutimiza azma ya muda mrefu ya Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp.
Dau la Uhamisho huu halikuvuka lile Dau la Rekodi ya Liverpool kumnunua Mchezaji kwa Bei Ghali ambalo waliliweka Mwaka 2011 walipomnunua Straika Andy Carroll kutoka Newcastle United.
Lakini Dau la Salah na Mchezaji mwingine wa Liverpool Sadio Mane anaetoka Senegal linalingana na kuwafanya ndio wawe Wachezaji wa Bei Ghali kutoka Afrika huko England.
Mwaka 2014, Liverpool walikosa kidogo tu kumnasa Salah aliekuwa Basle ya Switzerland na badala yake akatua Chelsea ambako alifeli kwa kwa kuanza Mechi 6 tu za Ligi Kuu England na kisha kutolewa kwa Mkopo huko Italy kwa Klabu za Fiorentina na AS Roma ambako Mwaka Jana alisaini Mkataba wa Kudumu kwa Dau la Pauni Milioni 15. Salah alikuwa mmoja wa walioisukuma AS Roma Msimu uliopita kushika Nafasi ya Pili kwenye Serie A nyuma ya Mabingwa Juventus kwa kufunga Bao 15 kwa Mechi 31.
Akiongelea Uhamisho huu, Jurgen Klopp ametamka: “Huu ni Uhamisho wa kufurahisha. Nimekuwa nikimfuatilia tangu aibuke huko Basle na amejengeka na kuwa Mchezaji Bora zaidi!”
Akiwa Liverpool, Salah atavaa Jezi Namba 11 iliyokuwa ikivaliwa na Roberto Firmino ambae sasa atavaa Namba 9. Salah anakuwa Mchezaji wa Pili kusainiwa na Liverpool katika kipindi hiki baada ya Chipukizi wa Chelsea mwenye Miaka 19 Dominic Solanke ambae Majuzi aliibeba England kutwaa Kombe la Dunia kwa U-20 huku yeye akiibuka Mfungaji Bora.
No comments:
Post a Comment