Pages

Saturday, June 17, 2017

Yaliyojiri Jioni ya Futari na Tuzo Simba


BEKI wa kushoto wa Simba Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amekabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora msimu wa 2016/17 wa timu hiyo katika hafla iliyofanyika katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
Zimbwe pia ndiye mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom msimu huo baada ya kucheza kwenye kiwango bora huku akifanikiwa kushuka dimbani katika mechi zote msimu mzima. Tayari Wekundu hao wameinasa saini ya beki Jamal Mwambeleko kutoka Mbao FC kwa ajili ya kumsaidia Zimbwe kutokana na kucheza mechi nyingi bila kumpumzika ambapo kwa sasa ni majeruhi.
Katika hafla hiyo mshambuliaji Moses Kitandu nae alikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora chipukizi. Kitandu alipandishwa kwenye kikosi cha wakubwa baada ya kuonyesha uwezo mkubwa akiwa na vijana (U20) lakini hata hivyo kocha Joseph Omog hakumpa nafasi kubwa ya kucheza.
Nae mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘MO’ amepewa cheti maalum kwa ajili ya kutambua mchango wake kwa timu hiyo katika masuala mbalimbali hasa yanayohusu fedha.
Mohamed Dewji ‘Mo’
MO alitoa sehemu ya pesa iliyosaidia kufanya usajili msimu uliopita huku pia akiungana na wanachama wengine kuchangia motisha kwa ajili ya wachezaji michango ambayo kwa namna moja au nyingine iliwafanya Wekundu hao kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi na kutwaa kombe la FA.

No comments:

Post a Comment