ARSENE WENGER ATAMANI UBINGWA BAADA YA KUSAINI MIAKA MIWILI
Mkataba huu, ambao hauna Kipengele cha Kuvunjwa, utamfanya Wenger adumu Arsenal kwa Miaka 23. Mara
baada ya Arsenal kutangaza kusainiwa kwa Mkataba huu, Wenger alitamka:
“Naipenda Klabu hii na naangaza ya baadae kwa matumaini makubwa na
msisimko mkubwa!”
Habari za ndani ya Arsenal zimedokeza kuwa Wenger atapewa Kitita cha Pauni Milioni 100 kusaini Wachezaji Wapya kwenye Dirisha la Uhamisho linalofunguliwa Julai 1.
Msimu
huu uliokwisha hivi karibuni, Arsenal walimaliza Nafasi ya 5 kwenye EPL
na hivyo kukosa kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao kwa mara ya
kwanza kwa Miaka 20 tangu 1996 Wenger aliposhika hatamu. Msimu ujao
Arsenal watacheza UEFA EUROPA LIGI nafasi ambayo wameiwini mara 2 kwa
kumaliza Nafasi ya 5 kwenye Ligi na pia kutwaa FA CUP walipowachapa
Mabingwa Wapya wa EPL Chelsea 2-1 kwenye Fainali iliyochezwa Wiki
iliyopita.
Licha kuwepo wasiwasi kuwa Wenger hatabaki Arsenal baada ya Mkataba wake kumalizika Juni hii, na hasa kusakamwa na Mashabiki wakitaka ang’oke, Bodi ya Arsenal, ikiongozwa na Mmarekani Arsene Stan Kroenke mwenye Hisa Aslimia 67, walitaka abaki.
Akiongea baada ya kuthibitishwa Wenger, Kroenke alinena: “Tunataka kutwaa Mataji, hilo ndio Mashabiki wanataka, Wachezaji, Wafanyakazi, Meneja na Bodi, wanataka na Wenger ndie bora kwa hilo!”
Nae Tajiri toka Russia, Alisher Usmanov, anaemiliki Hisa Asilimia 30 na ambae Wiki iliyopita alitoa Ofa ya Pauni Bilioni 1 kununua Hisa za Kroenke ametoboa kuwa anafurahi Wenger anabaki lakini anataka Bodi na Mmiliki Mkuu wa Hisa wamsapoti.
WENGER – HIMAYA YAKE:
-Kwenye Misimu yake 9 ya kwanza kuanzia 1996, Wenger alishinda Mataji Matatu ya EPL na FA CUP 4. -Msimu wa 2003/04, Wenger aliweka Rekodi ya kuwa Meneja wa kwanza kumaliza Msimu mzima bila kufungwa hata Mechi moja kwenye Ligi ya juu England.
-Lakini, baada ya kutwaa FA CUP Mwaka 2005, ukame ukatanda na akakaa Miaka 9 bila Kombe hadi 2014 alipotwaa FA CUP.
-Arsenal hawajakuwa Mabingwa wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, kwa Miaka 13.

Post a Comment