Pages
▼
Saturday, May 20, 2017
TIMU YA AZANIA YAKWEA PIPA KUELEKEA UINGEREZA
Timu ya Azania imeondoka nchini kuelekea Uingereza kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Standard Chartered Safari kwenda Anfield yatakayofanyika kwenye uwanja wa klabu ya Liverpool wa Anfield.
Timu hiyo imeondoka na msafara wa watu 10 ambapo kati yao wachezaji ni saba ambao ni Shabaka Hamisi, Rajabu Ally, Akhamedy Afifu, Abdala Khalidi, Thomas Bishanga, Alidi Said na Brayan Dobadi. Wachezaji wa Timu ya Azania wakibadilishana mawazo mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kukwea pipa kuelekea nchini Uingereza.[/caption]
Azania itashiriki mashindano hayo ikiwa ni mabingwa wa kombe la Standard Chartered Safari kwenda Anfield kwa Afrika Mashariki na Kati na ikiwa kwenye mashindano hayo itakutana na timu zingine kutoka Botswana, Nigeria, Hong Kong, Korea, Singapore, India pamoja na Uingereza.
Timu hiyo itafika Uingereza Mei, 19 wakiwa huko watakutana na timu zingine, Mei, 20 watatembelea uwanja wa Anfield, Mei, 21 watashuhudia mchezo wa Liverpool na Middlesbrough na baada ya hapo wataingia uwanjani kwa ajili ya mashindano na watarejea nchini Mei, 22. Mariam Sezinga (kushoto) wa Benki ya Standard Chartered Tanzania akiongoza msarafa huo wa timu ya Azania kuelekea nchini Uingereza Kikosi cha Timu ya Azania katika picha ya pamoja na kiongozi wa msafara huo Mariam Sezinga (wa kwanza kushoto) wa Benki ya Standard Chartered nchini kabla ya kuingia lango kuu la kusafiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Timu ya Azania wakiingia ku-'check in' tayari kukwea pipa kuelekea nchini Uingereza Mariam Sezinga (kulia) wa Benki ya Standard Chartered Tanzania akihakikisha hati zote zimekamilika tayari kwa ku-'check in' katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Timu ya Azania wakiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa Dubai usiku wa kuamkia leo safarini kuelekea nchini Uingereza
No comments:
Post a Comment