Pages

Friday, May 19, 2017

MAYANGA AITA 23 TAIFA STARS, DIDA NJE




KIPA wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ ameachwa katika kikosi cha wachezaji 23 wa Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kitakachoingia kambini Mei 23 kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Lesotho utakaochezwa Juni 10, Uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Akizungumza na wandishi wa habari leo Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga alisema alisema wachezaji wataingia kambini  na mazoezi yataanza Mei 24-29 Dar es Salaam na Mei 30 watakwenda kuweka kambi Misri kwa wiki moja.
“Baada ya mechi za mwisho za Ligi Kuu Tanzania Bara ambazo zitafika tamati wiki hii timu timu itaingia kambini Dar es Salaam kabla ya Mei 30 kwenda Misri kuweka kambi ya wiki moja itarudi Juni 7 kwa ajili ya mechi dhidi ya Lesotho,” alisema Mayanga.
Katika orodha ya majina ambayo Mayanga ametaja jina la Dida limeachwa na badala yake amechukuliwa kipa wa Yanga, Benno Kakolanya baada ya kufanya vizuri katika mechi za mwisho za Ligi Kuu na kuisaidia timu hiyo kutetea ubingwa.
Kikosi kamili cha Taifa Stars ni makipa Aishi Manula, Benno Kakolanya, Said Mohammed
Mabeki ni Shomari Kapombe, Hassan Kessy, Mwinyi Mngwali, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Salim Abdallah, Aggrey Morris, Abdi Banda na Erasto Nyoni.
Viungo ni Himid Mao, Jonas Mkude, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Said Ndemla, Muzamil Yassin, Simon Msuva, Farid Mussa (DC Tenerife), na Shiza Kichuya.
Washambuliaji ni Thomas Ulimwengu (FC Eskilstuna, Denmark), Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Mbaraka Yussuf, Ibrahim Ajib na Abdulrahman Mussa.
Benchi la ufundi ni Kocha Mkuu Salum Mayanga akisaidiwa na Fulgence Novatus, kocha wa makipa, Patrick Mwangata, Meneja ni Dani Msangi, Madaktari Gilberti Kigadiya na Richard Yomba na mtunza vifaa Ally Ruvu.

No comments:

Post a Comment