Dar es Salaam, May 20, 2017,
Baada ya kujitengenezea heshima
adimu kama ‘Prince wa Trap’ Tanzania kupitia ngoma yake, Pepeta, Chin Bees
ameachia wimbo mpya ‘Nyonga Nyonga’ pamoja na video yake.
Wimbo huo wenye mahadhi ya
dancehall iliyochanganyikana na ladha za aina yake za Kibongo, unadhihirisha
uwezo wa Chin katika kubadilika kwenye mahadhi mbalimbali kama atakavyo. Nyonga
Nyonga ambao ni wimbo wa pili wa rapper huyo akiwa chini ya usimamizi wa label
ya Wanene Entertainment.
“Ni dancehall lakini za watu fulani ambao
wamezimiss. Ni muziki fulani tofauti ambao hata mtu akisikiliza lazima
atabounce,” anasema. Ameongeza, “It’s a typical African hit na ikishakuwa hivyo
inaweza kusikilizwa kokote Afrika kwasababu nilichokifanya ni vitu ambavyo viko
musical, kote duniani wanaweza wakafeel. It’s a new tone,” anasema.
“Nimewaletea watu kitu ambacho
ni tofauti ambacho kitawafanya wacheze na mind zao ziwe fresh kwa kusikiliza.”
Wimbo huo umetayarishwa na Dr.Reggy,
mpishi ambaye amewahi kufanya miradi mingi na Chin Bees siku za nyuma. “Dr.Reggy
ni producer wangu wa kwanza kabisa, nimeanza kufanya naye kazi kitambo kabla
hata sijawa na jina kubwa,” anafafanua.
Video ya wimbo huo imefanyika katika
mitaa mbalimbali ya Dar es Salaam huku rangi za nguo walizovaa wote
wanaoonekana, zikitengeneza picha ya kuvutia machoni na yenye Uafrika mwingi.
Kuhusiana na video hiyo Chin
amesema, “Imefanyika hapa hapa Wanene na tuliamua kuifanyia nje zaidi tofauti
na video yangu iliyopita ya Pepeta ambayo yote ilifanyika ndani. Tumefanya kwenye
yale mazingira ya mtaani kabisa.”
“Theme ya video ilikuwa ni
kuonesha rangi za mtaani na mavazi pamoja na mazingira halisi ya Kitanzania na
yenye muonekano wa kizamani,” anasema Director H aliyeiongoza video hiyo.
Nguo hizo zimebuniwa na mbunifu
wa mavazi, Samuel Sebedayo (SAMZ) huku Rehema Samo akihusika kwenye styling.
Nyonga Nyonga ni wimbo
unaotarajiwa kuwa katika albamu ya kwanza ya Chin Bees iliyopangwa kuachiwa
baadaye mwaka huu.
Kuangalia video ya Nyonga Nyonga, bofya hapa: https://www.youtube.com/ watch?v=-z0HGHpMEwo&feature= youtu.be
Kupakua wimbo bofya hapa: http://bit.ly/ NyongaNyonga
KUHUSU CHIN BEES
Chin Bees ni rapper mwenye asili
ya Arusha aliyejizolea umaarufu kwa kipaji chake si tu katika kurap, bali pia
kuimba nyimbo za aina mbalimbali. Pamoja na nyimbo zake zikiwemo Pepeta, Zuzu,
Pakaza, Ruba na zingine kufanya vizuri redioni na kwenye runinga, ameshirikishwa
kwenye ngoma za wasanii wakubwa wakiwemo
Nick wa Pili na kushiriki kuandika nyimbo za wasanii kama Navy Kenzo na Vanessa
Mdee. Yuko chini ya usimamizi wa label ya Wanene Entertainment
KUHUSU WANENE ENTERTAINMENT
Wanene Entertainment kampuni ya
utayarishaji wa maudhui yenye studio za kisasa zaidi katika ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati na yenye makazi yake jijini Dar es Salaam. Imejikita katika
utengenezaji wa maudhui ya sauti, video na picha kwa kutumia wataalam waliobobea
katika sekta hiyo. Wanene imedhamiria kuleta mapinduzi katika burudani kwa
kutayarisha bidhaa zenye kiwango cha kimataifa.
No comments:
Post a Comment