SERENGETI BOYS YACHANGIWA SHILINGI MILIONI 12
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Harrison Mwakyembe jana alipokea kiasi cha sh milioni 12 kwa ajili ya timu ya
taifa ya vijana ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys.
Serengeti Boys iko nchini Gabon, ambako inashiriki mashindano ya 12 ya
Mataifa ya Afrika, Afcon 2017, ambapo juzi ilianza kwa suluhu dhidi ya mabingwa
watetezi Mali.
Fedha hizo ni sh milioni 10 kutoka kwa DStv na mil. 1 ya Taasisi ya
Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru),
ambazo zilikabidhiwa na
Mkurugenzi wa Maelezo, Hassan Abbas.
Pia Misa Tanzania nao walikabidhi sh milioni 1 ambayo ilitolewa na
mwenyekiti wake Salome Kitomari.
Waziri Mwakyembe aliwashukuru wote waliotoa michango hiyo na kuwataka
wadau kuendelea kuichangia timu hiyo, ambayo inawakilisha nchi katika
mashindano hayo ya Afcon 2017.
Aidha, Mwakyembe alisema kuwa wote walioichangia timu hiyo atawatangaza
katika magazeti ya Serikali ya Daily News na HabariLeo kama alivyoahidi awali
kuwa kila anayechangia atatangazwa.
No comments:
Post a Comment