WADAU WAOMBWA KUENDELEA KUICHANGIA SERENGETI BOYS
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Harrison Mwakyembe ameyataka makampuni na taasisi mbalimbali nchini kujitosa
kudhamini michezo.
Waziri Mwakyembe aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa
kuiaga timu ya Azania inayokwenda kushiriki fainali za Kombe la Standard
chartered zitakazofanyika wiki ijayo kwenye Uwanja wa Anfield, England chini ya
udhamini wa benki ya Standard Chartered.
Alisema kujitokeza kudhamini kutasaidia
kuhamasisha na kuinua michezo nchini.
Aidha, aliitaka timu hiyo kucheza kwa jitihada zote na kuhakiisha
inarejea na Kombe na anaamini kwa ubora iliyonayo, watarudi na ubingwa.
“Ni wakati wenu wa kwenda kuionesha dunia nzima kama mnaweza na mafanikio
yenu yatawatia moyo na vijana wengine," alisema.
Timu hiyo ambayo ni mabingwa wa Afrika Mashariki, ikiwa Uingereza
inatarajia kupambana na timu kutoka Botswana, Nigeria, HongKong, Korea, India
na wenyeji Uingereza.
Awali, Mjumbe wa bodi ya benki ya Standard Chartered Balozi Ammi Mpungwe
alisema ni mara ya kwanza kwa timu ya Tanzania kushiriki mashindano hayo na
anaimani na timu hiyo itatumia vyema fursa hiyo kuhakikisha wanarudi na
ushindi.
No comments:
Post a Comment