HATA kama
hautaki, Yanga ndio mabingwa wa msimu wa 2016/17 baada ya kuifunga Toto
Africans ya Mwanza kwa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Baada ya
ushindi huo Yanga imefikisha jumla ya pointi 68, ambazo zinaweza
kufikia wa Simba, lakini endapo tu Yanga watafungwa katika mchezo wao wa mwisho
dhidi ya Mbao FC mjini Mwanza Jumamosi.
Pamoja na
Simba kuwa na uwezekano wa kuifikia Yanga kwa pointi, lakini ni ndoto kwa timu
hiyo kuifunga Mwadui kwa zaidi ya mabao 12.
Yanga ina
mabao 57 ya kufunga na kufungwa 13, hivyo ina wastani wa mabao 44 wakati Simba
imefunga mabao 48 na imefungwa 16, hivyo ina wastani wa mabao 32 imepitwa na
Yanga kwa mabao 12.
Pamoja na
katika soka lolote linawezekana, lakini timu kufunga mabao 12 katika mchezo
mmoja ni jambo lisilowezekana kwani tangu msimu huu uanze, hakuna timu
iliyowahi kufunga zaidi ya mabao hayo.
Katika mechi
29, ambazo Simba tayari imeshacheza, haijawahi kushinda zaidi ya mabao matano,
hivyo timu hiyo tayari msimu huu imeshindwa kutwaa taji hilo.
Katika
mchezo huo wa jana, Amis Tambwe ndiye aliyeiwezesha Yanga kuondoka na pointi
zote tatu na kujihakikishia ubingwa mara ya tatu mfululizo baada ya kufunga bao
katika dakika ya 82 baada ya kupata pasi kutoka kwa Juma Abdul.
Vikosi
vilikuwa:-
Yanga:Beno
Kakolanya, Vicent Bossou, Juma Mahadhi/Kaseke, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kelvin
Yondani, Thaban Kamusoko, Haruna Niyonzima, Obrey Chirwa na Amis Tambwe.
Toto
Africans: Lucajo Lerient, David Kissu, Mohamed Soud, Hamimu Abdu, Ramadhani
Malima, Yusuph Mlipili, Carlos Protas, Juvenary Pastory/Waziri Ramadhani,
Hussein Kasanga na Waziri Junior.
Mechi
zingine za kufunga pazia la Ligi Kuu zitakazofanyika Jumamosi ni Azam FC
ataikaribisha Kagera Sugar, huku Majimaji atakuwa mwenyeji wa Mbeya City, Stand
United dhidi ya Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar na Toto Africans, Prisons dhidi ya
African Lyon na Ndanda itacheza na JKT Ruvu ambayo tayari imshashuka daraja.
No comments:
Post a Comment