MANCHESTER,
England
MANCHESTER City
wameanza fujo za usajili kwa kumpandisha ndege, kumfanyia majaribio na
kumsajili kiungo mshambuliaji wa Monaco, Bernardo Silva.
Katika dili la
pauni milioni 43.6, Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameanza kuonesha ni
aina gani ya kikosi anachokitaka kwa msimu wake wa pili hapo Etihad, akiwa
amemaliza huo wa kwanza pasipo kupata kikombe chochote.
Amemchukua
kiungo huyu mwenye umri wa miaka 22 baada ya kuwa amemsajili kinda mwingine Gabriel
Jesus kwenye eneo la ushambuliaji katikadirisha dogo la Januari, ambapo
alionesha kana kwamba alitaka kumweka kando Sergio Aguero.
Hata hivyo, sasa
amesema kwamba bado Aguero yumo kwenye mipango yake msimu ujao, ikielezwa
kwamba mpango ni kuachana na wachezaji wenye umri mkubwa na wasio na ufanisi
kadiri ya 10.
Silva ni raia wa
Ureno anayecheza kwa nguvu na yumo kwenye kikosi chaTimu ya Taifa ya Ureno.
Baadhi ya wachezaji wanaoondokani Jesús Navas,
Gaël Clichy, Willy Caballero na Bacary Sagna. Wengine walio kwa mkopo pia
waweza kuwa mwisho wao hapo City, nao ni Samir Nasri, Joe Hart, Eliaquim
Mangala na Wilfried Bony.
Manchester City
wataendelea kumwaga noti kuwanasa beki wa pembeni wa England na Tottenham
Hotspur, Kyle Walker na mlinzi wa Monaco, Benjamin Mendy.
No comments:
Post a Comment