LONDON,
England
LIVERPOOL
wapo tayari kuvunja benki ili wampate kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita.
Wekundu hao
wapo tayari kutoa pauni milioni 50 ili watengeneze kikosi kitakachofanya vyema
zaidi msimu ujao, ikizingatiwa kwamba Jurgen Klopp amewawezesha kuingia kwenye
Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL), baada ya kumaliza Ligi Kuu ya England (EPL)
wakiwa wkenye nafasi ya nne.
Wakitoa
pauni milioni 50 watakuwa wamevunja pia rekodi ya klabu hiyo, ambapo Leipzig
wameamua kumbandika mchezaji huyo bei hiyo ili kuwavunja matumaini ‘wachumba
tarajali’.
Liverpool
wanasema hiyo si kitu, na wapo tayari kuitupa mbali rekodi ya pauni milioni 38
walizotumia kumsajili And Carroll. Klopp anajipanga kuingiza majina makubwa
Anfield kiangazi hiki.
Mjerumani
huyo anaamini kwamba Keita, raia wa Guinea, ndiye mtu sahihi kwenye eneo la
kiungo, akiieleza Bodi ya Wakurugenzi Liverpool kwambandiye bora zaidi kwa
Ulaya sasa.
Kuna
uwezekano mkubwa kwa Liverpool kuvunja
rekodi ya matumizi yao yajumla ya fedha za usajili, kwani walitumia pauni
milioni 150, lakini sasa ikielezwa wanapanga kutumia kwenye pauni milioni 200
ili kwenda kwata moja na Manchester United na Manchester City. Keita atataka mshahara
wa pauni 120,000 kwa wiki.
No comments:
Post a Comment