Pages

Saturday, May 6, 2017

JKT RUVU YASHUKA RASMI DARAJA LEO



TIMU ya JKT Ruvu inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) imekuwa ya kwanza msimu huu kushuka daraja kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya leo kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Toto Africans.

JKT Ruvu imebakisha michezo miwili kabla ya kumaliza ligi hiyo, ambapo hata kama itashinda yote itafikisha pointi 30 ambazo haziwezi kuiokoa isishuke daraja.

Kwa mujibu wa kanuni za ligi hiyo msimu huu, timu tatu za mwisho ndiyo zinashuka daraja, ambapo timu zilizo na pointi ambazo JKT Ruvu inaweza kuzifikia ni Toto Africans yenye pointi 29 baada ya ushindi wa jana na Majimaji ya Songea pia yenye pointi 29, baada ya jana nayo kuifunga Mwadui.

Timu inayoshika nafasi ya nne kutoka chini ni Ndanda FC ya Mtwara yenye pointi 30, wakati African Lyon inashika nafasi ya tano kutoka mkiani ikiwa na pointi 31 sawa na Prisons iliyopo nafasi ya 10 ikiwa na pointi pia 31.

Kwa mazingira hayo baada ya JKT Ruvu kushuka daraja, hivi sasa timu za Majimaji, Toto Africans, Ndanda FC, Lyon na Prisons zitakuwa zikipambana kuepuka janga hilo na yoyote inaweza kuungana na JKT Ruvu.

Katika mchezo wa leo, JKT Ruvu ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya kwanza mfungaji akiwa Hassan Dilunga, kabla ya Toto kusawazisha dakika ya 20 mfungaji akiwa Waziri Junior kwa kichwa kutokana na krosi ya Mohammed Soud.

Dakika ya 35 Waziri Junior tena aliongeza bao la pili baada ya kutumia vizuri pasi ya Mohammed Soud.
Katika michezo mingine jana, Mwadui ilikubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Majimaji ya Songea, huku Ruvu Shooting na Kagera Sugar zikitoka sare ya bao 1-1.

No comments:

Post a Comment