USHINDI
wa mabao 2-0 ambao Yanga iliupata katika mchezo wake wa kiporo Ligi Kuu
Tanzania Bara dhidi ya Prisons Uwanja wa Taifa
Dar es Salaam, umeifanya timu hiyo ianze kupiga honi za kukaribia
ubingwa.
Yanga
imefikisha pointi 59 na kushika usukani wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiiengua
Simba yenye pointi 59 iliyokuwa inaongoza ligi kabla ya matokeo ya mechi hiyo
ya Yanga, ambapo Yanga ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Simba
yenyewe imecheza mechi 27 ikitarajiwa kushuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kesho kucheza na African Lyon katika mchezo wa raundi ya 28 ya ligi hiyo. Yanga
imecheza mechi 26.
Kutokana
na Yanga kuwa mechi moja ya kiporo kabla ya mechi ya Simba, huku pia ikiongoza
ligi hiyo, ina nafasi kubwa ya kutetea ubingwa, kwani ikishinda mchezo wake wa
kiporo itaizidi Simba pointi tatu.
Yanga
ikishinda michezo yake minne iliyobaki kabla ya kumaliza ligi hiyo itafikisha
pointi 72, wakati Simba yenyewe ikishinda michezo yake mitatu iliyobaki
itafikisha pointi 69.
Kwa
upande wa Simba yenyewe inaombea Yanga itoke sare michezo angalau miwili ama
itoke sare mmoja na kufungwa mmoja, huku yenyewe ikitakiwa kushinda michezo
yake yote ili kutwaa ubingwa huo.
Simba
ikishinda kesho dhidi ya African Lyon itarejea kileleni mwa msimamo wa ligi
hiyo kwa tofauti ya pointi tatu dhidi ya Yanga, lakini itakuwa inaizidi Yanga
michezo michezo miwili.
Katika
mchezo wa leo timu hizo zilienda mapumziko zikiwa hazijafungana, kabla ya mambo
kubadilika dakika 20 za mwisho, hasa baada ya kuingia Haruna Niyonzima badala
ya Said Juma ‘Makapu’ dakika ya 65.
Yanga
ilipata bao la kuongoza dakika ya 71 mfungaji akiwa Amis Tambwe akiunganisha
kwa kichwa krosi ya Juma Abdul, likiwa ni bao la 10 kwa Tambwe kwenye ligi hiyo
msimu huu.
Dakika
nne baadaye , Obrey Chirwa aliiandikia Yanga bao la pili kwa kichwa
akiunganisha mpira wa Tambwe. Bao hilo pia lilikuwa la 10 kwa Tambwe msimu huu.
Yanga:
Benno Kakolanya, Hassan Kessy/Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondan, Vincent Bossou,
Said Juma ‘Makapu’/Haruna Niyonzima, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi
Tambwe, Obrey Chirwa/Matheo Anthony na Geoffrey Mwashiuya.
Prisons;
Aaron Kalambo, Benjamin Asukile, Michael Ismail, James Mwasote, Nurdin Chona,
Jumanne Elfadhil, Salum Kimenya, Mohammed Samatta/Nchinjay Kazungu, Victor
Hangaya/Kassim Hamisi, Lambert Sibiyanka na Meshack Suleiman.
Wakati
huohuo, Simba leo itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Lyon, ambapo katika mchezo
wa kwanza msimu huu, Lyon ilishinda bao 1-0.
Ni
wazi Simba haitakubali kupoteza mchezo huo na kufifisha ndoto zake za ubingwa,
huku pia Lyon inayoshika nafasi ya 11 katika msimamo ikiwa na pointi 31 itataka
kushinda ili kujihakikishia kubaki Ligi Kuu msimu ujao.
No comments:
Post a Comment