Pages

Saturday, May 20, 2017

SERENGETI BOYS KIBARUANI KESHO




TIMU ya Taifa ya Vijana ya Tanzania, ‘Serengeti boys’ kesho inashuka uwanjani kucheza na Niger katika fainali za 12 za Afrika kwa vijana Uwanja wa Port Gentil, Gabon.
Awali Serengeti boys ilikuwa inacheza kwenye Uwanja wa Stade l’Amitie lakini Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limelazimika kuupeleka mchezo huo katika Uwanja wa Port Gentil, Gabon ili ichezwe kwa pamoja kutokana na ushindani uliopo kundi B
Mchezo huo ambao utaanza saa 12:30 saa za Gabon sawa na 2:30 usiku Tanzania utachezeshwa na mwamuzi Daniel Nii Ayi Laryea raia wa Ghana akisaidiwa na Seydou Tiama wa Burkina Faso na Mamady Tere wa Guinea.
Akizungumza kwa njia ya simu, Kocha Mkuu wa Serengeti boys, Bakari Shime maarufu kama Mchawi Mweusi, alisema mchezo huo ni muhimu kushinda ili kufuzu kucheza kombe la dunia.
“Tunamshukuru Mungu na Watanzania kwa sapoti yao ila naomba waendelee kutuombea kwani mchezo wa kesho (leo) ni muhimu kushinda ili kufuzu kucheza kombe la dunia,”
“Kauli mbiu yetu ni Gabon hadi kombe la Dunia na sisi Gabon tumefika sasa tunataka tufike India kwenye kombe la dunia,” alisema Shime
Pia Shime alisema baada ya kufanya vizuri michezo ya awali wachezaji wamepata ujasiri na mchezo na Niger wanaingia uwanjani wakiwa na lengo la ushindi tu.
Mchezo huu wa utatangazwa na radio Tanzania (TBC), radio one pia utaoneshwa Supersport nine na ZBC1.
Baada ya hatua ya makundi kumalizika timu mbili zitakuwa zimefuzu hatua ya nusu fainali na kukata tiketi ya kucheza fainali ya kombe la dunia kwa vijana waliochini ya miaka 17 zitakazofanyika nchini India baadae Oktoba.
Serengeti boys inahitaji sare tu kujihakikishia kufuzu nusu fainali na pia kufuzu Kombe la Dunia baada ya sare ya 0-0 na mabingwa watetezi, Mali na ushindi wa 2-1 dhidi ya Angola ambazo nazo zitacheza muda huo huo Uwanja wa Stade  l’Amitie mjini Libreville.
Serengeti boys ipo kundi B na timu za Mali, Niger na Angola na kundi A lina timu za Cameroon, wenyeji Gabon, Guinea na Ghana. 

No comments:

Post a Comment