JOSE MOURINHO AMSIFIA LUKE SHAW
Majuzi Mourinho alimponda Shaw kwa kutojituma na huku wengi wakidhani zama za Mchezaji huyo zimekwisha, Meneja huyo akamjumuisha kwenye Kikosi cha kuivaa Everton.
Jana Shaw, mwenye Miaka 21, alianza Benchi na kuingizwa Kipindi cha Pili kumbadili Ashley Young ambapo Shuti lake lililolenga Goli lilishikwa na Beki wa Everton Ashley Williams na kuzaa Penati ambayo Zlatan Ibrahimovic aliifunga katika Dakika ya 94 na kuipa Man United Sare ya 1-1.
Mbali ya Shaw, Mourinho pia alilalamikia baadhi ya maamuzi ya Mechi yao na Everton ya kukataliwa Bao zao 2 kwa Ofsaidi tata hasa lile la Ibrahimovic huku Paul Pogba na Ander Herrera wakipiga Posti.
Post a Comment